Back to photostream

Mch Michael Mgulu

Katika wiki ya pili ya ujenzi wa nyumba ya Ibada ya BCIC Maji Maupe (Maji Matitu) Mbagala Mch Michael Mgulu amesema na hapa namnukuu "Sisi hapa tulipofika katika maeneo haya, tukiwa hatuna fedha mkononi wala mfadhili kama ambavyo imezoeleka katika makanisa mengi na nchi mbalimbali, bali mfadhili wetu ni Mungu wetu maana wakati umefika ambapo Africa kuwa mfadhili wa mabara mengine duniani"

 

Afrika ni bara la misaada kwa wakati huu na ndivyo ilivyo makanisa na shughuli nyingi za kimaendeleo kama hivi mnavyoona leo tuko kwenye wiki ya pili ya ujenzi, hufadhiliwa na nchi wahisani.

 

Lakini sisi yote haya hakuna mhisani tunayemtegemea katika ujenzi, mishahara na mahitaji mbalimbali, tunamtegemea Mungu kwa asilimia mia moja.

 

Akaendelea kusema, wakati umefika muafaka kwa nchi zetu za Afrika kutoa misaada hata katika nchi za Ulaya na Mungu atatufungulia madirisha zaidi katika mapato, maono na kufanya yaliyo mbele zaidi.

1,073 views
1 fave
1 comment
Uploaded on May 17, 2010
Taken on May 16, 2010